
Kuanza duka la dawa muhimu (local pharmacy) kunahitaji kufuata taratibu maalum za kisheria ili kulinda afya ya wananchi na kuhakikisha bidhaa unazouza zina ubora unaokubalika.
Leseni ya biashara si tu huchangia kutambulika kisheria, bali pia husaidia kuepuka usumbufu wa kufungiwa biashara na kufungua fursa za huduma nyingine muhimu kama mikopo.
Faida za kuwa na Leseni ya Biashara
1. Hutambulisha biashara yako kisheria.
2. Huhitajika unapofungua akaunti ya benki ya biashara.
3. Hutumika kama nyaraka muhimu unapokopa fedha benki au taasisi za kifedha.
4. Huzuia usumbufu wa kufungiwa biashara.
5. Huchangia pato la Taifa kwa kulipa ada na kodi.
Hatua za Kupata Leseni ya Duka la Dawa Muhimu
1. Pata TIN kutoka TRA (Kama hauna tutakusaidia kuipata)
Ili kutambulika kama mlipa kodi, lazima upate namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN).
2. Usajili wa Kampuni (kama ni kampuni)
Ikiwa biashara yako inafunguliwa chini ya jina la kampuni, pata cheti cha usajili kutoka BRELA.
3. Mkataba wa Umiliki wa Eneo la Biashara
Wasilisha moja kati ya nyaraka hizi kuthibitisha umiliki au upangaji wa eneo:
Title Deed, Lease Agreement, Sales Agreement, Residential License
4. Kibali cha Mfamasia (Permit Award from Pharmacy Council)
Pharmacy Council inahitaji kila duka la dawa kuendeshwa chini ya usimamizi wa mfamasia aliyeidhinishwa. Ni lazima upate kibali hiki kabla ya kuanza biashara.
5. Vyeti vya Kitaalamu Kutoka TMDA
Kwa kuwa unauza dawa, lazima uwe na kibali kinachotolewa na TMDA (Tanzania Medicines and Medical Devices Authority) kinachothibitisha usalama na ubora wa bidhaa zako.
Ukikamilisha hatua zote na nyaraka kuthibitishwa, utapewa leseni yako ya biashara yenye muda wa matumizi wa mwaka mmoja.
Nyaraka Muhimu za Kuambatanisha
TIN namba (TRA), Cheti cha usajili wa kampuni (kama ipo), Mkataba wa pango/umiliki wa eneo, Tax Clearance Certificate (TRA), Kibali cha Mfamasia (Pharmacy Council), Kibali cha TMDA cha kuuza dawa muhimu
Kufuata hatua hizi kunahakikisha biashara yako ya kuuza dawa muhimu inaendeshwa kisheria na kwa usalama. Usipuuze hatua yoyote kwa sababu ukaguzi wa mara kwa mara hufanywa na mamlaka husika kama TMDA na Pharmacy Council.
Unahitaji msaada wa kupata leseni ya duka la dawa muhimu haraka bila usumbufu? Mimi na timu yangu tutakusaidia kushughulikia kila hatua ukiwa mahali popote Tanzania. Tuma ujumbe WhatsApp sasa hivi: +255693880325