
Kama unataka kuuza pombe au vinywaji vingine kwa rejareja (retail), jumla (wholesale), kuanzisha bar au kwenye grocery, ni lazima uwe na leseni halali inayokubalika kisheria.
Bila leseni hiyo, biashara yako iko hatarini kufungiwa, kutozwa faini. Leseni ya BAR, Grocery, na Liquor Store pamoja na masharti na nyaraka unazopaswa kuwa nazo.
1. Kuandaa Nyaraka Muhimu
Kabla ya kuomba leseni ya kuuza pombe na vinywaji, unatakiwa kuwa na nyaraka muhimu zinazokubalika kisheria. Nyaraka hizi ni pamoja na TIN (Taxpayer Identification Number) kutoka TRA, Cheti cha Usajili wa Kampuni (kama ni kampuni), pamoja na Tittle Deed, Lease Agreement, Sales Agreement au Residential License kuthibitisha umiliki au upangaji wa eneo utakaloendeshea biashara yako. Nyaraka hizi ndizo msingi wa kuonyesha kuwa biashara yako ipo halali na ipo katika eneo sahihi.
2. Kujaza Fomu ya Maombi ya Leseni
Utakwenda katika Halmashauri husika (kwa leseni ndogo) au BRELA (kwa leseni kubwa) kujaza fomu maalum ya maombi ya leseni ya biashara. Katika hatua hii utahitajika kuainisha aina ya leseni unayoomba, kwa mfano kama ni Retailer on bar au Sub-wholesale of liquor. (Hapa Victoria agency tunaweza kukusaidia kukamilisha usajili wako)
3. Kuambatanisha Vyeti vya Kodi na Vibali Vingine
Pamoja na fomu, unapaswa kuwasilisha Tax Clearance Certificate kutoka TRA ili kuthibitisha kuwa huna deni la kodi. Endapo biashara yako inahusisha bidhaa zinazodhibitiwa kama vile pombe, unatakiwa pia kuwasilisha vibali vya kitaalam vinavyohitajika kutoka mamlaka husika (mfano, TBS kwa ubora wa bidhaa). Hatua hii inalenga kuhakikisha bidhaa unazouza zinakidhi ubora unaokubalika kisheria.
4. Malipo ya Ada ya Leseni
Baada ya nyaraka zako kukaguliwa na kuidhinishwa, Afisa Biashara wa Halmashauri atakuandalia Bill ya Malipo kupitia mfumo wa mapato wa serikali za mitaa (Local Government Revenue Collection System). Utalipa ada hiyo kupitia benki kulingana na kiwango kinacholingana na aina ya leseni na eneo la biashara yako. Ada hizi hutofautiana kati ya miji, manispaa na wilaya.
5. Kupokea Leseni Yako
Mara baada ya kufanya malipo na kuthibitishwa, utapewa leseni yako ya biashara. Leseni hii inakuwa na taarifa muhimu kama namba ya leseni, jina la kampuni, TIN, eneo la biashara na muhuri wa mamlaka husika. Leseni hii hutumika kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe iliyotolewa na inapaswa kufanyiwa upya kila mwaka kabla ya kuisha muda wake.
6. Masharti ya Kuendesha Biashara Yenye Leseni
Unapopata leseni ya kuuza pombe na vinywaji, unatakiwa kuzingatia masharti kama vile kutoa risiti kwa kila mauzo, kuuza bidhaa zinazokubalika kisheria, na kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu. Kukosa kufuata masharti kunaweza kusababisha leseni kunyang’anywa na mamlaka husika.
7. Kwa Nini Leseni Hii ni Muhimu?
Leseni inakutambulisha kisheria na inakuepusha na usumbufu wa kufungiwa biashara. Pia inakusaidia kufungua akaunti ya biashara, kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha na kuaminika zaidi kwa wateja na washirika wa biashara.
Mimi na timu yangu tunasaidia wafanyabiashara kama wewe kukamilisha mchakato huu bila usumbufu. Tupigie simu au tuma WhatsApp kupitia wa.me/+255693880325 ili tukusaidie kufanikisha upatikanaji wa leseni yako kwa urahisi na haraka.