Jinsi ya kulinda biashara yako kwa kusajili jina la biashara

Kwanza kabisa, unatakiwa kuchagua jina la biashara yako. Kisha uhakikishe halijatumika na mtu mwingine. Ukipata jina jipya, linakuwa lako kisheria baada ya kusajiliwa. Endapo jina ulilotaka tayari limesajiliwa, utatakiwa kubadilisha na kuchagua lingine. Usajili huu ndio unakupa umiliki halali wa jina la biashara yako — hakuna mtu mwingine anayeweza kulitumia kiholela.
Taarifa Unazohitaji Kujaza
Unaposajili jina lako kupitia Mfumo wa Usajili wa ORS, unatakiwa kuweka:
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Namba ya simu
- Anwani ya sanduku la barua
- Anwani ya eneo la biashara na makazi
- Aina ya biashara unayofanya
Kwa maneno mengine, unatakiwa kuonyesha wewe ndiye mmiliki halali wa biashara hiyo na mahali inapopatikana.
Muda wa Kupata Cheti
Ukishawasilisha taarifa zako sahihi, ndani ya siku mbili pekee utakuwa umepata cheti chako cha usajili wa jina la biashara. Endapo kutakuwa na marekebisho, utapata mrejesho haraka ili uyafanye na kuendelea na hatua.
Utaratibu wa Kupokea Cheti
Baada ya maombi kukamilika, cheti chako kitapatikana moja kwa moja kwenye akaunti yako ya ORS — bila usumbufu, bila foleni. Taarifa zote kuhusu hatua za usajili zinatumwa kupitia barua pepe uliyoingiza.
Ada ya Utunzaji
Baada ya kusajili, jina la biashara linatakiwa kutunzwa kila mwaka kwa kulipia ada ndogo ya TZS 5,000 tu. Hii inahakikisha jina lako linaendelea kuwa mali yako halali na salama kisheria.
Victoria Agency tunakupa msaada wa haraka na rahisi: Kuanzia uchaguzi wa jina sahihi, maandalizi ya nyaraka, hadi kupokea cheti cha usajili, tutakuwa nawe kila hatua.
Piga simu au WhatsApp kwa +255693880325 ili uanze mchakato wa kusajili jina lako la biashara leo. Hakuna haja ya kungoja — biashara yako inastahili jina linalotambulika kisheria! #Tunasajilikampuni