
1. Leseni ya biashara ni nini?
Leseni ya biashara ni kibali cha kufanya biashara kinachotolewa na mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria ya Leseni ya Biashara Na.25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake.
2. Ni makundi gani ya leseni ya biashara yapo?
Kuna makundi mawili: Kundi A (biashara zenye mtaji mkubwa, hutolewa na BRELA) na Kundi B (biashara za kawaida, hutolewa na Halmashauri za Mitaa).
3. Leseni ya biashara hudumu kwa muda gani?
Leseni hutumika kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia tarehe ilipotolewa.
4. Faida za kuwa na leseni ya biashara ni zipi?
Kutambulika kisheria, kusaidia kufungua akaunti ya biashara, kutumika kukopa benki, kuepuka kufungiwa biashara, na kuchangia pato la taifa.
5. Ni nyaraka gani zinahitajika kuomba leseni?
- Hati ya TIN kutoka TRA
- Cheti cha usajili wa kampuni (kama ni kampuni)
- Mkataba wa pango (kama umepanga)
- Tax Clearance Certificate kutoka TRA
- Vyeti vya mamlaka husika kwa huduma za kitaalam (mf. TCRA, TBS, EWURA, TMDA, n.k.)
6. Ninawezaje kulipia ada ya leseni ya biashara?
Malipo hufanywa kupitia control number
7. Ada ya leseni ya biashara hupangwa vipi?
Inategemea aina ya biashara na eneo la Halmashauri (Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji), siyo ukubwa wa mtaji.
8. Je, leseni inaweza kufutwa?
Ndiyo, kama imepatikana kwa udanganyifu au mmiliki amekiuka masharti yake.
9. Ni vitu gani lazima viwe kwenye leseni ya biashara?
Namba ya leseni, aina ya leseni, jina la mamlaka, TIN, jina la biashara, eneo, ada iliyolipwa, namba ya stakabadhi na tarehe, sahihi na muhuri wa mamlaka.
10. Biashara gani zinahitaji leseni ya kundi A?
Biashara zenye mtaji mkubwa kama vile benki, bima, huduma za mawasiliano, bandari, utalii, na maduka ya kubadilisha fedha.
11. Biashara gani zinahitaji leseni ya kundi B?
Migahawa, hoteli za kawaida, wakala wa bima, vyama vya ushirika, usajili wa abiria, viwanda vidogo, udalali, na biashara za jumla/rejareja.
12. Ninawezaje kujua ada halisi ya biashara yangu?
Tutakwambia kulingana na mkoa, wilaya, ulipo
13. Ninaweza kupata leseni ikiwa niko mkoa mwingine tofauti na biashara ilipo?
Leseni hutolewa na mamlaka ya eneo ambalo biashara ipo, hivyo maombi yanapaswa kufanywa huko.
14. Sina uzoefu wa kupata leseni ya biashara, mnanisaidiaje?
Ndiyo, Victoria Agency tutakusaidia hatua zote kuanzia kujaza fomu, kukusanya nyaraka, mpaka kupata leseni yako.
15. Mkiwa Victoria Agency, mnaweza kunipatia leseni ikiwa mimi niko mbali?
Ndiyo, tunatoa huduma popote ulipo Tanzania, kwa mawasiliano ya simu au WhatsApp +255693880325
16. Ni nyaraka gani nitahitaji kuandaa kabla ya kuanza mchakato nanyi?
Tutakupa orodha kamili, lakini kwa kawaida ni TIN, cheti cha usajili (kama ni kampuni), mkataba wa pango na Tax Clearance.
17. Mnashughulikia leseni za aina zote?
Ndiyo, tunashughulikia Kundi A na Kundi B.
18. Ada za huduma zenu zinapangwa vipi?
Ada inategemea aina ya biashara na mkoa ulipo, na tutakujulisha kabla ya kuanza kazi.
19. Mnaweza pia kusaidia ku renew leseni?
Ndiyo, tunasaidia upyaishaji (renewal) pamoja na leseni mpya.
20. Ninawezaje kuwasiliana nanyi haraka?
Piga simu au tuma WhatsApp kwa namba +255693880325.